,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, June 15, 2017

Msanii wa muziki Nedy Music amefunguka kwa kudai kuwa sio kweli kwamba alitoa kauli ‘wasanii wa Zanzibar waache kulalamika’ ambayo ilitafsiriwa vibaya na baadhi ya wasanii hao.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Nedy Music alidai kauli ambayo aliitoa aliwataka wasanii wa Zanzibar kufanyakazi kwa bidii.
“Mimi sikusema waache kulalamika,” alisema Nedy “Niliwataka wafanyekazi kwa nguvu zao zote kwa sababu mbona kuna wasanii wa kule kipindi cha nyumba walifanya vizuri sana. Kwahiyo naweza kusema mimi sikuwaongelea vibaya nilikuwa nataka kuonyesha kila kitu kinawezekana hata huku bara kuna wasanii wengi wakali lakini hawafanyi vizuri,”
Alisema ingawa yupo chini ya label ya PKP ya Ommy Dimpoz lakini yeye binafsi nje ya label hiyo anajaribu kufanyakazi kwa bidii zaidi.
Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Dozee’.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi