,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, June 14, 2017

Msanii wa muziki wa asili, Saida Karoli amedai hajawahi kuzungumza na msanii wa Bongo Fleva, Darassa toka atumie baadhi ya vionjo vya wimbo wake, ‘Maria Salome’ kwenye wimbo ‘Muziki’

Muimbaji huyo ambaye katika wimbo wake mpya ‘Urugambo’ ametumia baadhi ya vionjo kutoka kwenye wimbo Salome wa Diamond, Muziki wa Darassa pamoja na ‘Give It To Me’ wa Belle 9, amekiambia kipindi cha Kwetu Fleva cha Magic FM kuwa kati ya wasanii hao, Belle 9 ndiye msanii ambaye yupo naye karibu zaidi.
“Darassa sijawahi kuongea naye lakini Belle 9 ni mtu wangu wa karibu sana na tumetengeneza nyimbo mbili ambazo kwa sasa hivi zipo tayari. Moja tumeshirikiana na Wara Wara (G  Nako) na Belle 9 ni ya kwetu wote watatu, na moja ni yangu mimi kama mimi, na wametoa ushirikiano mzuri,” amaesema Saida Karoli.
Kuhusu tetesi kuwa huenda akaja kuwa chini ya usimamizi wa lebo ya WCB, Saida amesema uongozi wa lebo hiyo haujawahi kumuambia kitu hivyo hizo zinabaki kama stori zisizo na ukweli wowote kwa sasa.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi