,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, June 13, 2017

Muimbaji wa muziki wa asili, Saida Karoli amedai ametumia vionjo vya wimbo wa Diamond na Belle 9 kwenye wimbo wake mpya ‘Urugambo’ baada ya waimbaji hao kutumia vionjo vyake katika nyimbo zao zilizopita.

Diamond alitumia vionjo vya wimbo ‘Maria Salome’ wa mkongwe huyo kwenye wimbo wake ‘Salome’ na Belle 9 pia alitumia vionjo vya wimbo huo huo kwenye wimbo wake ‘Give It To Me’.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Saida amesema alitumia vionjo vya wasanii hao baada ya waimbaji hao kuvitumia vionjo vya wimbo wake huo.
“Walitumia vionjo vya wimbo wangu wakijua mimi nipo hai ndio maana na mimi nikachukua vyao kama walivyochukua vyangu, nikatengeneza muziki na namshukuru Mungu umepokelewa vizuri sana,” alisema Saida.
Muimbaji huyo amedai alishindwa kurudi kwenye muziki kwa muda mrefu kutokana na kukosa menejimenti ya kuusimamiwa muziki wake.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi