,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, June 16, 2017

Msanii wa Hip Hop, Motra the Future amesema kundi la Weusi wamekuwa watu wa karibu sana katika muziki wake, huku akikanusha tetesi kuwa yeye na msanii Dogo Janja hawaelewani.

Rapper huyo amekiambia kipindi cha Kwetu Fleva cha Magic FM, baada ya kutoa wimbo na G Nako ‘Sina Koloni’ na kufanya vizuri, muda wowote anaweza kutoa wimbo na msanii mwingine kutoka Weusi kutokana na ukaribu wao.
“Weusi wale ni broo zangu, unaona ngoma kama Uswazi hadi nimeachia wale ndio wamesimamia kila kitu, wanasikiliza ngoma na kutoa mapendekezo na mimi ndio niko nao daily. Mipango ipo lazima kitokee kitu kingine kikubwa zaidi… ni yeyote yule ambaye atakuwepo kwa muda huo, inabidi tufanye kitu fulani,” amesema Motra.
Katika hatua nyingine Motra amesema yeye na Dogo Janja ni wa marafiki na wamekuwa wakitembeleana mara kwa mara wala hakuna kuchuniana kati yao  kama ilivyokuwa ikielezwa.
“Tunatembelea sana aisee!, hamna rafiki yangu kama yule hata jana nilikuwa nae, pia ninao machizi wangu wengi wa Dar wakina Zaiidi, Country Boy, OMG ni masela zangu wale wote,” ameeleza Motra.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi