,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Sunday, June 18, 2017

Msanii wa muziki wa hip hop, Roma Mkatoliki amewaahidi mashabiki wa muziki wake kuachia wimbo mpya muda wowote.

Rapa huyo na wenzake watatu walitekwa na watu wasiojulikana na kuteswa na baada ya siku tatu kutelekezwa katika eneo la Kunduchi Beach.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Roma alidai mashabiki wake wanasubiria vitu viwili muhimu katika muziki wake.
“Kwa sasa mashabiki wanataka wimbo wangu wa kwanza pamoja na show yangu ya kwanza. Watu wanajiuliza huyu jamaa anatakujaje baada ya matatizo. Hata nikiwa kwenye msiba watu wanazika wananiuliza vipi ngoma mpya mzee,” alisema Roma
Aliongea “Kwahiyo sitaki kukaa muda mrefu siku yeyote naachia wimbo mpya tena huwenda ikawa mwezi huu mtukufu kwa sababu kazi zipo tayari ni kupanga na kuamua kutoa kazi,”
Rapa huyo hivi karibuni alitembelea shule ya msingi Mchikichini Mbagala jijini Dar es salaam na kutoa msaada wa vifaa vya kujifunzia.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi