,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, June 14, 2017

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora, Angella Kairuki amesema kuwa tayari serikali imeshatoa kibali cha ajira 15,000 katika kujaza nafsi zilizoachwa wazi na Watumishi wenye vyeti fekiAmezungumza leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge Rita Kabati lililohoji,Je ni lini sasa zoezi la kuziba zile nafasi ambazo wale
wenye vyeti feki walioondolewa zitazibwa?“Kwanza naomba nimpongeze kwa kuwa amekuwa akifuatilia ajira kwa kuwa amekuwa akifuatilia ustawi wa watumishi lakini pia namna ambavyo amekuwa akifuatilia upungufu huu uliojitokeza katika zoezi la uhakiki wa vyeti feki nipende tu kusema kwamba tumekuwa tukieleza humu ndani tayari kibali cha ajira kimeshatolewa 15,000,” alisema Kairuki.
“Tulikuwa tunafanya mashauriano na ofisi ya Rais Tamisemi, wameshatuletea orodha maana yake tulitakiwa tujue kila kituo ni ninafasi ipi ambayo iko wazi nipende tu kusema katika maeneo yalioathirika sana ni sekta ya elimu na sekta ya afya kwa zaidi ya asilimia 70 na zaidi kidogo.”

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi