,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, June 13, 2017

Muigizaji wa Filamu nchini, Shamsa Ford amesema ni vigumu kwa mume wake ‘Chidi Mapenzi’ kuoa mke wa pili ingawa dini inamruhusu kwa sababu wote wawili kila mmoja anamuonea wivu mwenzake.

Shamsa Ford ameeleza kuwa suala hilo hawezi kabisa kwani katika wanawake watano wenye wivu duniani yeye ni mmoja wapo.
“Nahisi nitakufa, yaani siwezi na yeye mwenywe anajua siwezi. Na yeye mwenyewe mume wangu hawezi kwa sababu ana wivu kupitiliza, hawezi kumiliki mwanamke mwingine lakini akinipe reason za nguvu zikaonyesha kweli anahitaji mwanamke mwingine nitamruhusu, hivyo nitazoea kwa ajili ya Mwenyenzi Mungu,” Shamsa Ford ameimbia FNL ya EATV.
Katika hatua nyingine Shamsa ameongeza kuwa muda wowote anaweza kuongeza mtoto wa pili kwani mwanaye wa kwanza Terry ameshakua.
“Tena bahati nzuri I thanks God kupata mwanaume ambaye mtoto wangu ni rafiki yake, kwa hiyo wakikaa wenyewe wananiteta sana, sometime Rashid anamwambia Terry mwambie mama nataka mdogo wangu, na yeye anakuja mama nataka mdogo wangu, kwa hiyo wanahitaji na kwa nguvu za Mwenyezi Mungu atakuja,” ameongeza.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi